Mwakilishi wa wadi ya Bassi Bogitaorio, eneo bunge la Bobasi kaunti ya Nyamira, amefikishwa kotini kwa madai kuwa alitishia kumua bibi yake.
Bonface Okenye alifikishwa mahakamani siku ya Jumatano kwa madai kuwa alitishia kumtoa uhai mkewe Damaris Kwamboka.
Okenye alifikishwa mbele ya jaji John Njoroge ambapo alisomewa mashtaka kuwa katika mwezi wa Februari mwaka huu katika maeneo ya Jogoo alimtumia mkewe ujumbe akimtishia kumua.
Kwa upande wake Okenye aliyakana mashataka hayo ambapo aliachiliwa kwa bondi ya Sh 100,000.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe tatu mwezi wa sita.