Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi wa wadi ya Sensi eneo bunge la kitutu chache kaskazini Ochong’a Saisi amefadhili wanafunzi mayatima 400 kutoka wadi yake sare za shule pamoja na viatu.

Mwakilishi huyo aliwafadhili wanafunzi hao sare hizo na viatu siku ya Jumatatu katika eneo la Sombogo na eneo la Nyagesenda, huku akisema hiyo ndio njia mojawapo ya kuwawezesha mayatima hao kuenda shule ili kusoma na kuinua viwango vyao vya elimu katika wadi yake.

“Mayatima wengi huwa hawana wa kujali maslahi yao, nami kama mwakilishi wa eneo hili niliamua kuwafadhili mayatima wote ili wasome wasije wakasahaulika katika jamii ya eneo langu haswa kimasomo,” alidokeza Nyagaka.

Mwakilishi huyo aliwaomba mayatima hao kutia bidii katika masomo ili waje kujisaidia nyakati sijazo.

Wakati huo huo, wakaazi kutoka wadi yake walimpongeza kwa kuwakumbuka mayatima ambao wamekuwa tayari wasahaulika katika jamii

“Tunampongeza Mwakilishi wetu kwa usaidizi ambao ameanzisha kutoa katika wadi hii ya Sensi na tunamwomba aendelee kufanya hivyo kila wakati,” alihoji Clemesia Nyabuto, mkaazi.

“Tungekuwa na wawakilishi kama huyu katika wadi zote 45 katika kaunti ya Kisii, masomo yangeinuka zaidi na tunahitaji mayatima waendelee kusaidia maana hawana wazazi wa kujali maslahi yao,” alisema Cicilia Kerunda.

Aidha, wakaazi hao walimuomba mwakilishi huyo kuwakumbuka walemavu katika wadi yake, jambo ambalo mwakilishi huyo aliitikia na kusema alichaguliwa kuwafanyia maendeleo na wakaazi wote wa wadi yake huku akiahidi kufanya hivyo.