Mwakilishi wa watu walio na ulemavu katika bunge la kaunti ya Nakuru Emmah Mbugua sasa amekashifu muungano wa upinzani wa Cord kwa kufanya maandamano ya kutaka makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuondoka afisini.
Katika kikao na wanahabari Jumanne hii mjini Nakuru, Mbugua, kwa niaba ya walio na ulemavu kaunti hiyo ametaka muungano huo wa upinzani ukiongozwa na vinara wao Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula kukoma kuwashinikiza wafuasi wao kupiga kambi mbele ya afisi za IEBC na badala yake kufuata sheria zilizopo katika juhudi zao za kuwafurusha makamishna hao.
‘ IEBC ni tume huru na inatekeleza maswala yake kwa njia iliyo huru. Kwa niaba ya walio na ulemavu katika kaunti ya Nakuru, ningependa kusema kwa Raila na kundi lake, ikiwa IEBC inafaa kwenda nyumbani, kuna njia inayofaa kufuatwa. Kuna njia ya kutoa tume yoyote ile afisini,’ alikariri Mbugua.
Alitaka makamishna wa tume ya IEBC kuendelea kutekeleza majukumu yao hadi wakati ambapo muda wao afisini utakapokamilika au wakati ambapo sheria itafuatwa ya kuwaondoa afisini.
Wakati huo huo, Mbugua ameitaka tume ya uwiano na utangamano -NCIC- kutekeleza wajibu wao wa kuhakikisha kuwa kuna utangamano hapa nchini na kumchukulia yeyote nyule ayakayezua vuruga hapa nchini hatua kali.
‘NCIC, wafanye kazi yao. Yeyote atakayezua vurugu achukuliwe hatua kali. Hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria.
Kwa muujibu wake, wakati kunapotokea mizozo, walio na ulemavu, watoto na wanawake huadhirika pakubwa