Mwakilishi wa wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini Onchong’a Nyagaka amewakosoa baadhi ya wanasiasa ambao wanamlaumu kutokana na matokeo duni ya shule za wadi yake.
Akiongea na mwandishi huyu mjini Kisii, Nyagaka aliwakosoa baadhi ya wanasiasa hao dhidi ya kumhusisha kwa masuala ambayo hayajui, na kusema sekta ya elimu husimamiwa na serikali ya kitaifa.
“Sekta ya elimu husimamiwa na serikali ya kitaifa, wale ambao wananilahumu kuwa shule za wadi yangu hazijafanya vyema katika mitihani nawaomba wakome kwani kazi yangu ni kuhakikisha nimefanya maendeleo kwa kuwakabidhi wanafunzi pesa za 'basari' ili waendeleze masomo,” alisema Nyagaka.
Nyagaka aliomba wazazi kushirikiana na walimu ili kuinua viwango vya elimu katika shule za wadi hiyo kuliko kusikiliza wanasiasa wanao endeleza siasa zisizo sheheni maendeleo.