Vijana katika wadi ya Kivumbini, Nakuru hatimaye wana kila sababu ya kutabasamu baada ya mwakilishi wadi hiyo Vitalis Okello kuahidi kufanya kazi na vijana.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza Alhamisi katika mkutano na vijana, Okello alisema kuwa swala la ukosefu wa ajira ni changamoto Kwa vijana na hata serikali kuu. 

Hata hivyo, alidokeza kuwa kando na hayo, atazidi kuhakikisha vijana wa wadi ya Kivumbini wanapata manufaa kutokana na tenda za kaunti ya Nakuru. 

Alitoa wito kwa vijana kujiunga katika vikundi na hata kusajili kampuni ili kunufaika na tenda hizo Kwa urahisi.

"Shida kubwa ya vijana ni ukosefu wa ajira, lakini tukijiunga Kwa vikundi mbalimbali tutapata usaidizi hata kutoka serikali ya kaunti na hii ni kupitia ofisi yangu," alisema Okello.

Wakati huo huo aliongeza kuwa bajeti ya mwaka wa kifedha 2016/2017 vijana wameangaziwa mno na hivyo basi wanafaa kujipanga.

Mwakilishi wadi Vitalis Okello katika mkutano wa vijana.Amekariri kufanya kazi Kwa karibu na vijana ili waweze kujiiimarisha. PMambili/Hivisasa.com