Mwakilishi wa Wadi ya Kongowea Jabez Odour ameitaka Serikali ya Kaunti ya Mombasa kutimiza ahadi zilizowekwa kwa wakaazi wakati wa uchaguzi uliopita.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea mjini Mombasa siku ya Alhamisi, katika eneo la Maweni, Wadi ya Kongowea, Oduor alisema kuwa bado sehemu nyingi katika maeneo ya wadi hiyo zinakumbwa na tatizo la miundo msingi duni, licha ya serikali ya kaunti kuahidi kutekeleza miradi.

Mwakilishi wadi huyo alisema kuwa hali mbaya ya barabara imetatiza shughuli za uchukuzi pamoja na zile za kimasomo kwani huwa ni vigumu kwa watoto kufika shuleni kwa wakati ufao.

Oduor alidai kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa serikali ya kaunti chini ya uongozi wa Gavana Hassan Joho imeshindwa kuwajibikia majukumu yake kikamilifu.

Aidha, amewataka wakaazi kujitenga na viongozi walio na ahadi za uongo, akisema kuwa ndio wanaozidi kurudisha nyuma maswala ya maendeleo mashinani.

"Tafadhali wakaazi msiwahi kuwachagua viongozi wasiojali matatizo yenu, kwani kazi yao ni kutoa ahadi za uongo,” alisema Jabez.