Mwakilishi wa Wadi ya Shanzu Maimuna Salim ameitaka Mahakama ya Mombasa kusikiliza na kuamua kwa haraka kesi ya ufisadi inayomkabili.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Salim anataka kesi hiyo isikilizwe na kuamuliwa kabla ya uchanguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2017.

Kupitia wakili wake Oduory Simiyu, Salim aliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo ili apate fursa ya kugombea kiti cha uwakilishi wa wadi wa Shanzu.

Hayo yamejiri baada ya Hakimu Susan Shitubi kuahirisha kesi hiyo iliyotarajiwa kusikizwa Jumatatu kwa kutaja sababu zisizoweza kuepukika.

Salim anadaiwa kupokea hongo ya shilingi milioni 1.5 kutoka kwa Leah Aketch ili kumsaidia kutatua mzozo wa ardhi baina ya yake na serikali ya Kaunti ya Mombasa mnamo Julai mwaka jana.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 26 mwezi Aprili.