Mwakilishi wadi huyo alisema kuwa kila mkenya ana uhuru wa kujistarehesha na kileo anachotaka. [Picha/ capitalfm.co.ke]
Mwakilishi wadi mteule katika bunge la Kaunti ya Mombasa Fatma Kushe amesema kuwa atawasilisha mswada wa kutaka biashara ya shisha kuhalalishwa katika kaunti hiyo.
Kushe alisema kuwa wafanyabiashara wa shisha wanapswa kuruhusiwa kuendeleza biashara yao hasa katika maeneo yaliyoidhinishwa na serikali ya kaunti ya Mombasa.
Kauli yake inajiri siku chache baada ya serikali kuu kupiga marufuku utumizi na uagizaji wa shisha kote nchini.
Kwenye ripoti yake, Kushe alisema kuwa kila mkenya ana uhuru wa kujistarehesha na kileo anachotaka, na kuikosoa vikali hatua ya serikali kupiga marufuku utumiaji wa shisha.
“Wizara ya Afya inapaswa kuheshimu sheria ya ugatuzi na kutambua kuwa kila serikali ya kaunti ina uhuru wa kuidhinisha sheria za kuwalinda wakaazi wake,” alisema Kushe.
Kauli yake inakinzana na ya viongozi mbalimbali na wanaharakati wa kupambana na mihadarati katika Kaunti ya Mombasa ambao walipongeza hatua hiyo ya serikali ya kupiga marufuku utumizi wa shisha.
Aidha, wanaharakati hao wameitaka serikali ya kitaifa pia kupiga marufuku utumizi wa miraa.
Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6