Mwakilishi wa eneo wadi ya Gesima Ken Nyameino amejitokeza kushtumu muungano wa Cord kuhusiana na mpango wa muungano huo kutaka kuwashinikiza makamishna wa tume ya IEBC kuondoka afisini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu mapema Jumatatu, Atuti alisema kuwa mipango ya muungano wa Cord inaenda kinyume na sheria za nchi.

“Hivi vitisho wanavyovitoa vinara wa Cord havina msingi na nikinyume na sheria za taifa hili kwa maana iwapo tume hiyo imeshindwa kutekeleza majukumu yake kuna bunge linalostahili kuwachunguza makamishna hao na kisha kuchukua hatua mwafaka,” alisema Nyameino.

Atuti aidha aliwataka vinara wa muungano wa Cord kuiruhusu tume hiyo kutekeleza majukumu yake bila kuingisha siasa kwenye masuala ya usimamizi wa tume hiyo.

“Ni ombi langu kwa vinara wa muungano wa Cord kuepukana kabisa na masuala ya kuingisha siasa kwenye usimamizi wa tume ya IEBC kwa maana tume hiyo ni huru," aliongezea Nyameino.