Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa wadi ya Airport Ibrahim Omondi al-maarufu kama Bomoa, amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta.Omondi anadaiwa kumuita Rais Kenyatta 'caretaker president' mnamo Oktoba 19, 2017 katika jengo la Bunge la Kaunti ya Mombasa.Omondi aidha anakabiliwa na shtaka la pili la kutangaza kuwa hakutafanyika marudio ya uchaguzi wa urais katika Kaunti ya Mombasa.Hata hivyo, mwakilishi wadi huyo alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Francis Kyambia siku ya Jumatatu.Hakimu Kyambia ameagiza Omondi kuachiliwa kwa dhamana ya shillingi 200,000 ama shillingi 100,000 pesa taslimu.Omondi alitiwa mbaroni usiku wa kuamkia Ijumaa wiki iliyopita, na kuzuiliwa korokoroni kwa siku tatu.Kesi hiyo itatajwa tarehe Novemba 17, 2017.