Share news tips with us here at Hivisasa

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Bobembe wilayani Nyamira, alifikishwa mbele ya mahakama moja mjini Nyamira siku ya Alhamisi na kushtakiwa kwa kosa la kumnajisi mwanafunzi wa darasa la saba.

Akiwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama hiyo Tranford Maati, mshtakiwa Daniel Matara, alisomewa shtaka hilo analo daiwa kulitekeleza mnamo tarehe Julai 3, 2015.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alimnajisi mwanafunzi huyo katika nyumba yake na kumtishia maisha iwapo angemwambia yeyote.

Mwalimu huyo alikanusha shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh90,000 ambapo kesi hiyo itasikizwa tena tarehe Novemba 2, 2015.