Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ya Mombasa imemhukumu mwalimu wa dini ya Kiislamu kifungo cha maisha gerezani kwa kupatikana na kosa la ulawiti.

Mshtakiwa huyo, Yusuf Ahmed Yusuf, mwenye umri wa miaka 52, amepatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa umri wa miaka tisa mnamo tarehe 1 mwezi Machi, katika eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mshukiwa aliwaagizia wanafunzi waende kucheza na kisha kubaki nyuma na mlalamishi kabla ya kumtendea uovu huo.

Akitoa uamuzi huo siku ya Ijumaa, Hakimu Richard Odenyo alisema kuwa ushahidi uliotolewa unatosha kuthibitisha mshukiwa alitekeleza kitendo hicho.