Mwalimu wa dini aliyefungwa miaka 20 jela kwa kosa la kutoa mafunzo ya itikadi kali kwa wanafunzi wa shule ya msingi amekata rufaa kupinga kifungo hicho.

Share news tips with us here at Hivisasa

Salim Mohamed, al maarufu kama Samuel Wabwire, alikata rufaa hiyo siku ya Jumanne, mbele ya Hakimu Dora Chepkwonyi.

Mahakama ya Mombasa ilimuhukumu kifungo cha miaka 20 gerezani mwezi Januari mwaka huu, baada ya kumpata na hatia ya kutoa mafunzo ya itikadi kali kwa watoto wachanga.

Wabwire anadaiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali kwa watoto sita wa Shule ya msingi ya Gotani, iliyoko kaunti ya Kilifi kati ya Januari 8 mwaka 2013 na Jan 19, 2015.

Jaji Chepkwonyi alikubali rufaa hiyo ilicha ya kuwasilishwa ikiwa imechelewa.

Kulingana na sheria, rufaa inafaa kukatwa chini ya siku 14 baada ya hukumu kutolewa.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 18 mwaka huu.