Nur Adan Mohammed akiwa katika Mahakama ya Mombasa siku ya Ijumaa. [Picha/ barakafm.org]
Mwalimu mmoja wa dini ya Kiislamu alifikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa siku ya Ijumaa kujibu shtaka la ulawiti.Nur Adan Mohammed anadaiwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 13 katika madrasatul Alfalaha Al-Islamiah iliyoko eneo la Majengo Mapya, huko Likoni.Mohammed anaidaiwa kutekeleza kitendo hicho mnamo Disemba 5, mwaka huu.Aidha, alishtakiwa kwa madai ya kumshambulia mtoto huyo na kumsababishia majera kati ya mwezi Mei na Disemba mwaka huu.Hata hivyo, Nur alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Edgar Kagoni na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja.Kesi hiyo itasikilizwa mnamo Januari 15, 2018.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6