Mwana wa mshukiwa mkuu wa dawa za kulevya Ibrahim Akasha na wenziwe wameonywa dhidi ya kukwepa vikao vya kesi inayowakabili.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Hakimu Julius Nangea alisema iwapo washukiwa hao watakosa vikao vya kesi hiyo, basi dhamana yao itafutiliwa mbali ama kuwekewa masharti makubwa.

Hii ni baada ya Ibrahim Akasha kukosa kuhudhuria kikao cha kesi hiyo juma lilopita, kwa kusema kuwa alikuwa amelazwa hospitalini.

Huku hayo yakijiri, mahakama imeagiza kuendelea kusikizwa kwa kesi ya kuwasafirisha nchini Mariakani washukiwa hao.

Baktash Akasha, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha na Vijaygiri Goswami wanakabiliwa na madai ya ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya heroini.