Mwendeshaji wa bodaboda mjini Nyamira ametiwa mbaroni baada ya kumnyanganya afisa wa polisi bunduki yake.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Nyamira, mkuu wa polisi katika kaunti hiyo Ricah Ongare alisema kuwa mwanabodaboda huyo alikuwa akigombana na afisa wa polisi katika baa moja mjini humo.
Ongare aliongeza kuwa wawili hao walikuwa wakipigania msichana na kwa bahati mbaya mwanabodaboda huyo akamzidi nguvu afisa wa polisi na kumnyanganya bunduki.
Ongare alisema walipata bunduki kutoka kwa mwanabodaboda huyo siku ya jumatatu na kumtia mbaroni.
"Mwanabodaboda huyo atafikishwa mahakama kwa kosa la kumnyanganya afisa wa polisi bunduki yake na kosa la kupigana na afisa wa polisi,” alisema Ongare.
“Tumepata bunduki ya afisa huyo baada ya kumkamata mwanabodaboda huyo,” aliongeza Ongare.
Kulingana na mkuu huyo wa polisi Richa Ongare mwendeshaji huyo atafikishwa mahakamani kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya dhidi ya afisa wa serikali.