Mahakama kuu jijini Mombasa imemuhukumu kifo, mwanachama wa vuguvugu la MRC anayekabiliwa na mauwaji ya aliyekuwa mlinzi wa gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Faraji Konde Kazungu anakabiliwa na madai ya mauwaji ya askari Harisson Maitha mnamo Oktoba 4, 2012.

Aidha, anakabiliwa na madai mengine ya kupanga kuvuruga uchaguzi na mtihani wa kitaifa wa mwaka 2013.

Jaji Martin Muya kutoka mahakama kuu ya Mombasa, alisema kuwa kulingana na utafiti wa chembe chembe za DNA zilizopatikana kwenye suruale na kisu zinaambatana na zile za mwendazake pamoja na mshukiwa, ishara tosha kuwa alihusika pakubwa katika mauwaji hayo.

Jaji Muya, alimuhukumu kifo na yuko na siku 14 za kukata rufaa.

Wakati uo huo mahakama imewaachiliwa huru wenzake Omari Diofu Gwashe, Suleiman Mohamed na Justus Randu Nyundo waliokuwa wanakabiliwa na madai sawia na hayo.