Mwanachama wa halmashauri ya kupambana na mihadarati NACADA, Sheikh Juma Ngao anamuomba kukutana na raisi Uhuru Kenyatta ili kujadili swala sugu la dawa za kulevya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ngao amesema dawa za kulevya zimekithiri katika ukanda wa pwani hasa miongoni mwa vijana wadogo.

Aidha, ameongeza kuwa kuna baadhi ya wageni wamechangia kuingizwa kwa dawa hizo humu nchini.

Akizungumza na mwanahabri huyu, Ngao ameitaka serikali kuhakikisha ukaguzi wa mizingo kutoka nje ya nchi inakaguliwa kwa hali ya juu, ili kuzia biashara za mihadharati.

“Visa vya uhalifu vimeongezeka hasa pwani kutokana na ongezeko la vijana wanaotumia mihadarati," alisema Ngao.

Siku ya Jumatano, Ngao alisisitiza kuwa itakuwa vyema iwapo kutajengwa kituo cha kurekebisha tabia kwa wanawake wanaotumia mihadarati eneo la Pwani.