Mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza katika Shule ya Kijue eneo la Likoni, amefariki baada ya kupigwa na nguvu za umeme siku ya Jumatatu.
Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi katika eneo la Likoni, Willy Simba, alisema kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa huenda mwanafunzi huyo alikanyaga nyaya ya umeme zilizokuwa zimeangushwa na mvua kubwa iliyokuwa imenyesha siku ya Jumapili.
Hata hivyo, Simba alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kwa kuwashirikisha maafisa wa kampuni ya umeme nchini, ili kubaini haswa nini kilichosababisha kifo hicho.
Hata hivyo, Wakaazi wa Likoni wamelaumu maafisa kutoka kampuni ya umeme ya KPLC kwa kuzembea kazini na kusema kuwa familia ya mwanafunzi huyo lazima ifidiwe.