Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanafunzi wa shule moja ya upili iliyoko Nakuru alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kwa madai ya kuzua vurugu na kwa kutumia lugha ya matusi.

Wycliff Mbuya, mwenye umri wa miaka 22, anadaiwa kuvuruga amani na pia kumtusi Cyrus Njiramba katika duka lake mnamo Oktoba 14, 2015.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa mshtakiwa alitumia majina ya matusi mbele ya wateja wa mlalamishi.

Mbuya hata hivyo alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkuu Liz Gicheha na kujitetea kuwa yeye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Uamuzi wa kesi hiyo utatolewa tarehe Novemba 12, 2015.