Baada ya kumaliza mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka jana, anaonekana mcheshi, mchangamfu akiwa na matumaini ya kujiunga na shule tajika nchini Kenya.
Natasha Moraa kutoka kijiji cha Mwochiri, wadi ya Marani, Kisii aliona ndoto yake kutimia baada ya kuibuka mwanafunzi wa pili katika shule ya msingi ya kisii na alama 357. Ama kweli mchumia juani hulia kivulini.
Moraa anatoka katika familia maskini lakini hilo halikumvunja moyo. Natasha, ukimtizama kwa sasa anatiririkwa na machonzi na mwenye kupoteza matumaini Baada ya kukosa nafasi katika shule ya wasichana ya Chogoria baada ya wazazi wake kukosa kuimudu karo.
Wanafunzi wenzake wanaendelea na masomo lakini yeye bado yupo nyumbani. Natasha alishindwa kuzungumza na hivi sasa kwa kushidwa kustahimili machungu yaliyomzidi, badala yake alitiririkwa na machonzi.
Steve Maraga aliyekuwa mwalimu wake wa Kiswahili alisema kuwa wazazi wa Moraa ni maskini sana na pia ni wagonjwa na hizi ndizo shida zinazomzuia kuenda shule.
Maraga alisema kwa sasa Moraa amezongwa na mawazo asijue la kufanya. Kupitia kwa walimu wake, anaomba wasamaria wema kujitolea ili wamsaidie kujiendeleza kimasomo.