Mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili jijini Mombasa amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kuuza pombe.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mwanafunzi huyo alitiwa mbaroni na maafisa wa polisi katika shule moja ya upili iliyoko Mikindani, akiwa na chupa ya kileo aina ya changaa.
Mshatakiwa alikubali mashtaka hayo mbele ya Hakimu Daglous Ogoti siku ya Alhamisi.
Mwanafunzi huyo aliambia mahakama kuwa anafanya biashara hiyo ili kukimu maisha yake pamoja na ndugu zake wadogo kwani mama yao amelazwa katika Hospitali ya Portreitz.
“Nafanya kazi hii ya kuuza pombe ili niweze kulipa gharama ya hospitali ya mamangu na kukimu mahitaji ya ndugu zangu wadogo. Naomba msamaha na msada tafadhili,” alisema kijana huyo.
Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 19, mwaka huu.