Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanahabri wa gazeti la The Star Malemba Mkongo pamoja na muhariri wa gazeti hilo, wameagizwa kufika mahakamani kujibu madai ya kuandika kuwa kulipatikana bomu ndani ya jengo la mahakama kuu ya Mombasa.

Malemba aliandika taarifa kuwa kulipatikana bomu ndani ya jengo la mahakama ya Mombasa mnamo Disemba 10,2015 wakati kesi ya wasichana wanne wanaokabiliwa na madai ya ugaidi ilipokuwa ikiendelea.

Aidha, Malemba aliandika kuwa aliambiwa na afisa wa kupambana na ugaidi ATPU kuwa anashuku wafuasi wa Al-shabab walihusika katika uekeja wa bomu hiyo.

Haya yalijiri siku ya Jumatano baada ya wakili wa wasichana hao, Hamisi Mwadzogo kuwasilisha ombi katika mahakama kuu kutaka kuchukuliwa hatua za kisheria mwanahabari huyo pamoja na muhariri wa gazeti hilo, kwa kile alichokitaja kuwa kuhujumu haki za wateja wake na utendakazi mzima wa mahakama kuhusu kesi inayowakabili wateja wake.

Taarifa hiyo imechapishwa katika gazeti la The Star la Jumatano katika ukurasa wa tatu.

Malemba pamoja na muhariri wa gazeti hilo wanatarajiwa kufika mahakamani Disemba 29, 2015 kujibu madai hayo.