Mahakama kuu jijini Mombasa imetoa onyo kwa mwanaharakati Mgandi Kalinga dhidi ya kuendelea kutuma jumbe za matusi kwa Seneta mteule Emma Mbura.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jaji katika mahakama kuu ya Mombasa Patrick Otieno, alimwagiza Kalinga siku ya Alhamisi kukoma kutuma jumbe hizo ili kutoa nafasi kwa kesi yake kukamilika kwa haraka.

Haya yanajiri baada ya Seneta Mbura kupitia wakili wale Christine Kipsang, kuithibitishia mahakama kuwa bado mwanaharakati huyo angali anatuma jumbe hizo kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Jambo hilo lilipingwa na wakili wa Kalinga, Leonard Shimack, aliyesema kuwa hiyo ni hatua ya kuhujumu haki za mteja wake ikizingatiwa simu yake bado inazuiliwa na polisi.

Kalinga alishtakiwa kwa madai ya kutuma ujumbe wa sauti akimtusi Seneta Mbura katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp mwezi Machi mwaka uliopita katika eneo lisilojulikana.