Mwanaharakati wa Nakuru David Kuria kutoka shirika la Nakuru Human Rights Network NAHURINET amepinga vikali hatua ya Rais kusema kuwa Kenya itajiondoa mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya ICC.

Share news tips with us here at Hivisasa

katika mahojiano na mwanahabari huyu Jumanne afisini mwake, Kuria alisema kuwa kujiondoa Kwa Kenya sio suluhu.

Aliongeza kuwa mahakama ya ICC imesaidia kurejesha nidhamu miongoni mwa viongozi. Kwa mujibu wake,kesi zilizotamatika mbele ya mahakama hio zilisaidia pakubwa kuepuka machafuko sawia mwaka wa 2013.

"Kwa upande wangu,siungi mkono Hata Kenya kujitoa katika mahakama ya ICC,ila kilichopo no viongozi kujali matamshi yao na kuepuka kujihusisha na machafuko,"alisema Kuria.

Wakati huo huo, aliwataka viongozi kuheshimiana na kuhubiri amani miongoni mwa makabila ya humu nchini.