Afisa wa masuala ya haki na sheria katika Shirika la Haki Afrika amesema kuwa makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, waliokubali kuondoka afisni hawafai kushtakiwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Ijumaa, Francis Gamba alisema hatua iliyochukuliwa na makamishna hao wa IEBC kuondoka afisini kwa hiari ni hatua mwafaka.

Gamba aliwakosoa baadhi ya wanaharakati wanaoshinikiza makamishna hao kufunguliwa mashtaka, akieleza hofu kuwa iwapo suala hilo litatiliwa mkazo basi huenda likaibua utata.

"Kuwashtaki makamishna hao sio jambo mwafaka kwani huenda likasababisha uhasama kutokana na kuwa wamewajibikia majukumu hata kama wengi wa Wakenya hawakubaliani nao. Sioni kama hatua hiyo ndiyo njia bora ya kutatua swala hili kwa sababu wamekubali kuondoka kwa hiari,” alisema Gamba.

Haya yanaarifiwa huku ripoti ya kamati ya pamoja iliyopewa jukumu la kuifanyia mageuzi Tume ya IEBC ikijadiliwa bungeni.