Kijana akitumia dawa za kulevya. [Picha/ allafrica.com]
Mwenyekiti wa shirika la Maaruf Anti-drugs Famau Mohammed Famau ameipongeza serikali kwa juhudi zake za kupambana na janga la mihadarati eneo la Pwani.Akizungumza na waandishi wa habari, Famau alisema kuwa vita dhidi ya mihadarati vimefaulu pakubwa kwani utumizi wa dawa za kulevya umepungua.“Serikali imejaribu sana kwa kujitahidi kuangamiza janga hili la dawa za kulevya eneo zima la Pwani,” alisema Famau.Hata hivyo, Famau alisema kuwa kuna haja ya juhudi za kupambana na mihadarati kuzidishwa maradufu ili kuweza kurudisha hadhi ya eneo la Pwani.Wakati huo huo, Famau ameupongeza mradi wa serikali wa Methadone wa kuwatibu waathiriwa wa mihadarati unaoendelea katika kaunti mbalimbali za Pwani.“Dawa za Methadone zimesaidia pakubwa na sasa vijana wengi wamejinasua kutoka kwa utumizi wa dawa za kulevya,” alisema Famau.Wakati huo huo, amewaonya vijana dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa kuvuruga amani.