Mwanaharakati wa Nakuru Masese Kemunche kutoka shirika la Centre for Enhancing Democracy and Good Governance CEDGG ameshtumu vikali wamiliki wa vyombo vya habari Kwa kutojali maslahi ya wanahabsri humu nchini.
Katika kikao na wanahabari Jumanne mjini Nakuru wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Masese alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wanawahangaisha wafanyikazi.
Alisema kuwa wanahabari wanatekeleza wajibu mkuu na wanafaa kutambuliwa na waajiri wao na hata kuwatunuku.
"Wengi wa wanahabari wanapitia masaibu si haba katika vyumba vya habari manake wanafanya kazi nzuri lakini kulipwa inakuwa balsa,"alisema Masese.
Wakati huo huo alidokeza kuwa uhuru wa wanahabari unafaa kuheshimiwa kwani ukiukwaji wake ni kinyume cha katiba inayotambua hilo.
Kwa mujibu wake,Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu katika maendeleo ya taifa hili.