Mwanaharakati Kalinga Mgandi akiwa kizimbani hapo awali. [Photo/ standardmedia.co.ke]
Mwanaharakati mmoja kutoka Mombasa amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kubomoa ukuta wa shule moja huko Likoni.Mwanaharakati huyo, Kalinga Mgandi, anadaiwa kubomoa ukuta wa Shule ya msingi ya Dena Olinda iliyoko katika eneo la Mtongwe. Ukuta huo unadaiwa kugharimu shiling 350,000. Wakati huo huo, Mgandi anakabiliwa na shtaka la pili la kuchochea umma kuzua fujo katika eneo hilo la Mtongwe.Hata Hivyo, Mgandi alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Evans Makori siku ya Alhamisi.“Sio ukweli, hiyo ni njama ya kuniharibia jina,” Mgandi aliambia mahakama.Hakimu Makori aliagiza mwanaharakati huyo kuzuiliwa korokoroni hadi siku ya Jumatatu, mjadala wa kupewa dhamana utakapo sikizwa. Hii ni baada ya afisi ya mwendesha mashtaka kutoa aombi la Mgandi kuzuiliwa baada ya kukwepa kesi mbili zinazomkabili eneo la Mariakani.