Mkurugenzi mkuu wa shirika la Nakuru Human Rights Network David Kuria ameunga mkono sheria mpya zilizotangazwa na mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kuria anasema kuwa sheria hizo ikiwemo kuondoa magari yaliyo na honi za kelele ni juhudi za kurejesha nidhamu.

"Naunga mkono NTSA kwa sheria hizo mpya manake nidhamu sasa itakuwa kwenye barabara zetu" Kuria alisema.

Wakati huo huo ametoa wito kwa mamlaka ya NTSA kuhakikisha kwamba wanashirkiana na maafisa wa trafiki ili kurejesha nidhamu hio barabarani.

Kwa mujibu wake, maafisa wa trafiki wana wajibu mkubwa katika kuhakisha hilo.

"Hizi sheria zote ni nzuri lakini bila ushirikiano wa trafiki itakuwa vigumu" Kuria alisema.

Mwanaharakati huyo ametoa wito kwa washikadau wote kushirikiana na mamlaka ya NTSA ili kuleta nidhamu inayostahili barabarani.