Mwanakamati wa hazina ya ustawishaji maeneo bunge wa eneo bunge la Magarini, Rashid Irengi Kariuki amefikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kuchukua fedha za hazina hiyo kinyume cha sheria.
Siku ya Jumatano, Mahakama ilielezwa kuwa kati ya Machi 16, 2010 na Septemba 16, 2010, Rashid Irengi Kariuki na Martha Wanagare Mureithi wanadaiwa kuchukua shilingi laki mbili na elfu ishirini na tisa kutoka kwa hazina za eneo bunge la Magarini.
Rashidi alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu Diana Mochache na kupewa dhamana ya shilingi milioni moja ama dhamana ya pesa taslimu shilingi laki tatu.
Wakati uo huo mahakama imetoa agizo la kukamatwa kwa Martha Wanagare Mureithi kwa kukosa kufika mahakamni ili kufunguliwa mashtaka sawia na hayo.
Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 4, 2016.