Mwanamke mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani na Mahakama kuu ya Mombasa, baada ya kupatikana na kosa la kumuua mke mwenza.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa, Doris Kawira, alihusika katika mauaji hayo bila kukusudia, baada ya kumdunga kisu Issabel Karim, katika eneo la Ziwa la Ng’ombe mnamo Januari 10, 2012.

Akitoa uamuzi wake siku ya Jumatano, Jaji wa Mahakama kuu ya Mombasa Martin Muya, alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wanane, unaonyesha kuwa Bi Kawira alihusika katika mauaji hayo.

Bi Kawira alipewa siku 14 kukata rufaa kupinga uamuzi huo kwa mujibu wa katiba.