Mwanamke anayedaiwa kumkata mumewe sehemu za siri na kupelekea kufariki kwake, ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshtakiwa huyo, Pauline Mukiri, anadaiwa kumkata mumewe, Allou Matata, sehemu za siri mnamo Februari 27, 2016 katika eneo la Bamburi.

Mukiri alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Susan Shitub siku ya Jumatatu.

Akitoa uamuzi wake, Hakimu Shitub alimuachilia mshukiwa huyo kwa dhamana ya shilingi laki tano.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe Mei 26, 2016.