Jaji wa Mahakama kuu ya Mombasa Mugure Thande ameagiza mwanamke anayedaiwa kumua bwanake na mtoto wao, kupelekwa katika Hospitali kuu ya Mkoa wa Pwani ili kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.
Mshtakiwa, Diana Kwamboka, anadaiwa kumua mumewe Juma Mohamed na mtoto wao Brandy Juma kati ya tarehe 8 na 9 mwezi Aprili katika eneo la Swabina Likoni, Kaunti ya Mombasa.
Aidha, Jaji Thande alimuagiza kiongozi wa mashtakasiku ya Jumatatu kumpa mshukiwa wakili atakaye mwakilisha katika kesi hiyo.
Kwamboka ataregeshwa mahakani tarehe 23 mwezi Mei kusomewa ripoti kutoka kwa daktari kabla ya kushtakiwa kwa mauaji.