ADVERTISEMENT
Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know
Mwanamke mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kupatikana na dawa za kulevya.
Mshtakiwa, Beatrice Awino, anadaiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi yenye thamani ya shilingi 1500.
Bi Awino alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Douglas Ogot siku ya Jumatano.
Mahakama iliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 21 mwezi Juni.