Mwanamke mmoja ameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kupatika na dawa za kulevya.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa huyo, Levina Oundo, anadaiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi yenye thamani ya shilingi elfu moja, tarehe 17 mwezi wa Aprili katika eneo la Changamwe, Kaunti ya Mombasa.
Mshukiwa huyo alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Irene Ruguru.
Hakimu Ruguru aliagiza kesi hiyo kusikizwa tarehe 7 mwezi Juni.