Mwanamke mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kuuza pombe kinyume cha sheria.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mshtakiwa, Zipporah Mgoti anadaiwa kupatikana akiuza pombe katika eneo la Mikindani, Kaunti ya Mombasa, baada ya masaa halali.
Bi Mgoti anadaiwa kupatikana akiuza pombe hiyo saa sita usiku.
Mshtakiwa huyo alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Daniel Ogoti.
Hakimu Ogoti aliagiza mshukiwa huyo kuregeshwa mahakamani siku ya Jumatano kusomewa hukumu yake.