Mama mmoja mwenye umri wa makamo amezua kioja nje ya Mahakama Kuu ya Kisii baada ya kupanda kwenye mti na kutishia kujirusha iwapo Mahakama hiyo haitamsikiliza.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mama huyu ambaye alitambuliwa kwa majina kama Mwende wa Kalekye kutoka Kaunti ya Machakos, alisababisha msongamano wa magari katika barabara hiyo ya RAM Hospital kuelekea kwenye Mahakama hiyo ambapo umati mkubwa wa watu walikitaka kujionea kilichojiri huku wengine wakimdhania kuwa na akili isiyotimia.

Kulingana na Afisa mmoja wa Polisi anayemjua huyo na hakutaka kutajwa jina alisema kuwa huyo amekuwa akitaka kuwasilisha kesi katika Korti hiyo dhidi ya Afisa mmoja wa Polisi, lakini amekuwa akizuiliwa kuingia humo ndani kwa kudaiwa anatumia utaratibu mbaya kuandikisha malalamiko yake.

Mama alisikika akiwataja baadhi ya Maafisa Wakuu wa Polisi na kusema kuwa antaka aruhusiwe kumuona Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo Kisii.

Hata hivyo, kilio cha mama huyo hatimaye kilisikilizwa ilipombidi Afisaa mmoja wa Mahakama hiyo kuingilia kati na kumbembeleza ashuke kabla ya kuandamana moja kwa moja na Afisa huyo hadi majengo ya Mahakamani ili kushughulikiwa alivyotaka.