Mwanamke mwenye umri wa makamo amefikishwa mahakamani kwa kumsaidia bintiye kuavya mimba.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kanze Changawa, alikubali kutekeleza kosa hilo mnamo Disemba 13, mwaka jana, katika eneo la Malomani.

“Ni kweli nilimsaidi mwanangu kutoa ujauzito wake,” alisema Kanze.

Hakimu katika Mahakama ya Kilifi Leah Juma ameagiza mwanamke huyo kuzuiliwa katika gereza la Shimo la Tewa mpaka pale mwendesha mashtaka atakapokamilisha ripoti yake kuhusu hali ya afya ya mtoto huyo aliyeavya mimba.

“Mama huyu atazuiliwa katika gereza la Shimo la Tewa, mpaka ripoti ya afya ya mtoto itakapoletwa,” alisema Hakimu Juma.

Aidha, ameagiza msichana huyo kuzuiliwa katika kituo cha kulinda watoto cha Malindi.