Mwanamke mmoja amefikishwa mahakamani baada ya kudaiwa kutekeleza wizi katika duka la jumla la Nakumatt, tawi la Likoni.
Naomi Njeri Mwangi, anadaiwa kutekeleza wizi huo usiku wa sherehe za kukaribisha mwaka mpya.
Mwangi anadaiwa kuiba lita tano za mafuta ya kupika, paketi mbili za maziwa, taulo ya kupanguza uso na vitu vingine, vyote vikiwa na thamani ya shilingi elfu 49.
Hata hivyo, mwanamke huyo alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Julius Ogoti.
“Sikuiba chochote, hizo ni porojo za kunisingizia,” alisema Mwangi.
Mahakama imemuachilia kwa dhamana ya shilingi laki mbili na mdhamini wa kiasi kama hicho.
Kesi hiyo itasikizwa Januari 17, mwaka huu.