Mwanamke mmoja amefikishwa kizimbani kwa kosa la kujaribu kumtupa mtoto mdogo mwenye umri wa miezi saba.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Shantel Matano, anadaiwa kujaribu kumtupa mtoto huyo mnamo Julai 23, mwaka huu katika eneo la Tudor, Moroto.

Bi Matano alikanusha shtaka hilo mbele ya Hakimu mkuu katika Mahakama ya Mombasa Teresia Matheka siku ya Jumatano.

Matano alizua kilio na kuitaka mahakama kumjulisha mtoto wake aliko.

Hatua hiyo ilifanya mahakama kuahirisha kikao cha kesi hiyo na kuiagiza afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa kufafanua alikopelekwa mtoto huyo.

Akizungumza na wanahabari nje ya mahakama, mwendesha mashtaka Erick Masila alisema kuwa mtoto huyo alipelekwa katika nyumba ya watoto ya Mji wa Salama iliyoko eneo la Tudor.

“Mtoto huyo yuko salama. Kwa sasa anapata hifadhi katika nyumba ya watoto ya Mji wa salama,” alisema Masila.