Aliongeza kuwa watu wawili kutoka hotelini humo walimdunga kisu mara kadhaa jambo lililopelekea kwake kufariki papo hapo. [Picha/Pngtree]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamme mwenye umri wa miaka 21 alidungwa kisu na kufarika Alhamisi eneo la Likoni mjini Mombasa kwa kile kinachodaiwa kuwa alikuwa na deni ya shilingi 10.

Mwanamme huyo aliyetambulika kwa jina moja kama Mike alifariki baada ya kupoteza damu nyingi kifuani na shingoni kwa sababu ya kutokana na unyama aliotendewa na washukiwa watatu.

Polisi wanasema kuwa kijana huyo alikuwa amekula chakula katika hoteli moja na kushindwa kulipa deni ya shilingi kumi na kuongeza kuwa tayari washukiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

Mkuu wa polisi eneo la Likoni Benjamin Rotich alisema kuwa marehemu alimaliza kula chakula ndani ya hoteli hiyo na baadaye kusema kuwa hakuwa na pesa ya kulipa deni hilo.

Aliongeza kuwa watu wawili kutoka hotelini humo walimdunga kisu mara kadhaa jambo lililopelekea kwake kufariki papo hapo.

‘‘Baada ya kula, alshindwa kulipa pesa hizo na kukawa na mvutano na majibizano kabla ya vita kuzuka ambapo alidungwa kisu na kufariki,’’ alisema Rotich.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha hospitali kuu ya pwani.