Mwanamme mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kujifanya polisi na kuwalaghai wananchi.
Siku ya Jumatatu, mshtakiwa kwa jina Ibrahim Hassan Yusuf alikubali mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu Teressia Matheka kabla ya kuhumiwa kifungo hicho.
Shtaka la kwanza ni kwamba anadaiwa mnamo Agosti 3,2015, katika eneo la vyemani gatuzi dogo la likoni kaunti ya Mombasa alijiwasilisha kwa njia ya udanganyifu kama mfanyi kazi wa serikali katika cheo cha afisaa wa polisi mbele ya Rama Shaaban Said.
Shtaka la pili ni kwamba mnamo Agosti 13,2015, akiwa eneo la Vanga huko Likoni kaunti ya Mombasa aliweza kumuibia Rama Shaaban simu aina ya Samsung Galaxy yenye thamani ya shillimgi 22,000 na pesa taslimu shilingi 8,000.