Mwanamme mmoja huko huko Turbo amewashangaza wakwe zake kwa kulipa shilingi mia nane kama mahari. Gabriel Mabonga aliwashtua wakwe zake baada ya kutoa shilingi mia nane kwa bahasha na kuwakabidhi. Dinah Nasike, aliyezipokea hizo pesa, alighadhabishwa sana na kitendo hicho. 'Hizi si pesa ambazo mtu anaweza kuwapa wakwe zake!' alisema kwa hasira. Hela hizo zilikuwa zalipwa, kabla ya Mabonga kumchukua mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na miwili ili akapelekwe kufanyiwa tohara. Mama Dinah mwenye hasira ilibidi atulizwe na wazee waliokuwa wakihudhuria kikao hicho baada ya kutishia kwamba angempeleka Kotini ili alipe pesa alizotumia kumlea yule mtoto. 'Mimi nimemtunza huyu mtoto tangu awe mdogo, halafu mtu ananiletea vijipesa ambavyo haviwezi hata kununua kiatu cha mtoto', alisena Nasike. Nasike alizidi kuongeza kwamba, mila zao haziruhusu thamani yoyote chini ya ng'ombe watatu ya kumlipia mtoto wa kiume kama mahari. Hata hivyo, pande zote mbili ziliafikiana baada ya muda mrefu wa mazungumzo. Hata hivyo, Nasike amesisitiza kwamba iwapo Mabonga hatafanya walivyokubaliana, basi hatakuwa na budi ila kumfikisha Kortini na alipie thamani ya malezi ya mtoto huyo kulingana na sheria.
UASIN GISHU
Mwanamme alipa shilingi 800 mahari
ADVERTISEMENT
Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-Ndiema