Mwanaume mmoja wa umri wa miaka 57 kutoka kijiji cha Kiabira, lokesheni ya Nyakware wilaya ya Nyamira alipatikana amejitia kitanzi nyumbani mwake Jumatano asbuhi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akithibitisha kisa hicho, naibu wa chifu wa lokesheni hiyo ya Nyamware Charles Nyameiyo alisema kuwa mwanamume huyo amekuwa akilala peke yake kando na mkeo kwa mda mrefu.

Wakati huo huo, naibu chifu aliongezea kuwa alipashwa habari kutoka kwa mke wa mwendazake kuwa alimpelekea uji asubuhi, na kumpata amejitia kitanzi.

“Huyu mama aliniambia hajui kilichosababisha mzee wake kujitoa uhai, na akasema alienda penye analala na akapata hayuko, ndio akaenda akampata amening’inia kwa chumba kingine tofauti kando na kile analala,” alitaja chifu Nyameiyo.

Mwili wa mwenda zake ulipelekwa chumba cha kuhifadhi maiti cha Nyamira, huku uchungunzi ukiendelea kuhusu swala hilo.

Chifu huyo amewaomba wakaazi wa eneo hilo kutojitia kitanzi wanapokuwa na shida yeyote, huku akisema ni busara kuleta jambo ambalo limesumbua kwa watu ili litafutiwe suluhu mwafaka kwani kujitoa uhai si suluhisho.

“Naomba kila mtu akumbuke kuwa maisha ni kitu ambacho kikienda hakirudi, naomba kila mtu kutafuta mbinu mbadala jambo mbaya linapotokea,” aliongezea Nyameiyo.