Majambazi waliokuwa wamejihami kwa bunduki walivamia boma la mzee mmoja katika kijiji cha Bokeira usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa na kumuua mzee wa boma hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Majambambazi hao walimfiatulia risasi tatu na kumuua papo hapo mzee huyo, huku wakimjeruhi mke wake na watoto kwa kuwamwagia kemikali za sumu. 

Mwili wa mzee huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Nyabondo na majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Nyabondo.

Afisa mkuu wa polisi katika kaunti ya nyamira Onunga amethibitisha hayo na kusema kuwa walioteleza unyama huo wanasakwa na watatiwa mbaroni.

"Maafisa wetu wa CID wameanzisha uchunguzi kuwasaka majangili hawa ambao wameteleza unyama huu," alisema afisa huyo.