Mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo aliwashangaza wakaazi wa kijiji cha Nubya alipotoa nguo zake nakusalia na suti ya Mungu.
Inasemekana mwanamme huyo aliyejulikana kwa jina Tuntera, alikuwa akielekea katika mji wa Kisii alipopatwa akiwa uchi.
"Nilimuona akikimbia huku akiwa uchi nakupiga kamsa natukaanza kumfuata ilitumkamate lakini tukashindwa kwani alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi sana," alisema Bw Calvin Ratemo ambaye ni jirani yake.
Wengine waliamua kuelekea nyumbani kwake walipopata vijiti vya bangi vilivyokuwa vimetumika.
Mke wake kwa upande wake aliwaeleza kuwa alikuwa kwenye shughuli za jioni alipomuona mme wake akitoroka nyumbani.
"Nilijaribu kumuomba arudi lakini sikuweza kwani alinishinda nguvu nakutoroka," alisema mke wake.
Hata hivyo majirani wake Bw Tuntera walisema kuwa alipogundua kuwa alikuwa uchi alijificha nakuamua kurudi nyumbani masaa ya usiku nakusema kuwa hatawai kuvuta bangi tena.
Majirani walipozidi kumuuliza maswali kuhusiana na kisa hicho, Bw Tuntera aliamua kuwafurusha kutoka Nyumbani kwake.