Kijana mwenye umri wa miaka 26 ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja kwa kosa la kumbaka na kumuoa mwanafunzi wa miaka 16.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshtakiwa, Amos Mutie, anadaiwa kutekeleza vitendo hivyo kati ya Septemba 2015 na Mei mwaka huu, katika eneo la Likoni.

Bwana Mutie anadaiwa kumuoa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya msingi ya Likoni, kisha kumtorosha hadi kaunti ya Makueni ambako amekuwa akikaa naye kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mshtakiwa huyo alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Mombasa Teresia Matheka siku ya Jumatano.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe Mei 26, 2016, ambapo mashahidi watano wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.