Picha ya gari moshi. [indiarailinfo.com]Jamaa wa umri wa makamo anayedaiwa kuwa mlevi ameaga dunia baada ya kugongwa na gari moshi eneo la Bogogoni eneo bunge la Changamwe.
Mwanamume huyo aliyetambulika kama Nyamawi alipaliwa alipokuwa amelewa nyakati za saa tisa alfajiri usiku wa kuamkia Ijumaa.
Kulingana na walioshuhudia wanasema mwendazake alizidiwa na pombe na akajilaza kwenye barabara ya reli, hali iliyosababisha kukanyagwa na treni hiyo.
Akithibitisha kisa hicho, siku ya Ijumaa, mama mtaa wa eneo hilo, Margaret Nyangasi amesema kuwa hiyo sio ajali ya kwanza kufanyika mahali hapo.
“Hii si ajali ya kwanza kama hiyo kutokea eneo hili,kuna zingine kama tano zilitokea awali”,alisema Margaret.
Amewataka wanao uuza pombe nyakati za usiku eneo hilo kuzifunga biashara zao, ili kuepeka maafa zaidi.
“Uuzaji wa pombe usiku kama huo,unafaa kukomeshwa eneo hili,ndio watu wengine wasigongwe na magari moshi”,alisema Magret.