Mwanamume mmoja amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nane katika jengo la NSSF jijini Mombasa.
Mwendazake, Mohamed Ali, ambaye alikua akifanya kazi ya kinyozi katika eneo la Kibokoni, alikuwa amemtembelea daktari katika jumba hilo kabla ya kukumbana na mauti yake.
Omar Mohamed, mmoja wa familia ya Ali, alisema mwendazake alikuwa anakabiliana na msongo wa mawazo.
Mwendazake tayari amezikwa kulingana na tamaduni za dini ya Kiislamu.